18 Aprili 2025 - 20:48
Source: IQNA
Jihad Islami: Hatuwezi chini silaha maadamu ardhi za Palestina zinakaliwa kwa mabavu

Makundi yote ya Palestina yameungana katika upinzani wao mkali dhidi ya pendekezo la kuzitaka harakati za Kiislamu za kupigania ukombozi (Muqawama) kuwaka chini silaha, afisa wa harakati ya Jihad Islami amesema.

Ali Abu Shaheen, mwanachama wa ofisi ya kisiasa ya harakati hiyo ya Jihad ya Kiislamu, amesisitiza kuwa silaha za Muqawama ni mali ya watu wa Palestina.  

Alitoa kauli hiyo katika hotuba yake Jumatano jioni, aliongeza kuwa mpango wa utawala wa Israeli wa kuachana na silaha za Muqawama haukubaliki.  

Amesema maadamu ardhi za Palestina zinakaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni, hakuna kundi lolote la Wapalestina litakalokubali kuachana na silaha, alisema.  

Silaha za makundi ya upinzani ni suala la heshima na imani na zinaonyesha historia ya mapambano dhidi ya wavamizi wa Israeli na makundi yote ya Wapalestina.  

Mahmoud Mardawi, mwanachama mwandamizi wa Hamas, pia alikataa wazo la kuachana na silaha, akielezea kuwa silaha za Muqawama ni maisha ya watu wa Palestina.  

"Hakuna kurudi nyuma. Hatutawahi kujadiliana kuhusu silaha zetu na wale wanaozibeba katika hatua yoyote," alisema.  

Wakati huo huo, Vikosi vya Kitaifa na Kiislamu vya Palestina vilitoa taarifa, vikisema, "Tunapinga vikali kupokonywa silaha harakati za Muqawama. Mpango huo unalenga kuharibu silaha za msingi ambazo Wapalestina hutumia tu kwa kujilinda, wakati huo huo Marekani inaripotiwa kupeleka shehena kubwa ya silaha hatari na mabomu mazito kwa Wazayuni ili kuzitumia dhidi ya taifa la Palestina lisilo na ulinzi."  

Kamati hiyo ilisisitiza kuwa kukuzwa suala la kupokonywa silaha harakati za Muqawama ni upotoshaji kwa sababu tatizo linahusiana na kushindwa kwa Wazayuni kutekeleza makubaliano ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza, makubaliano ambayo upande wa Palestina ulikubali na kuzingatia.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha